Friday, March 7, 2014

ULIMISS HII? MACHANGUDOA WAFANYA PATI YA KUSHEREHEKEA KUFANYA NGONO BILA KONDOMU, KISA DAWA YA UKIMWI IMEPATIKANA

Posted by Edwin Moshi On Saturday, December 07, 2013
Ikiwa ni siku kadhaa zimekatika tangu kutolewa kwa taarifa ya kupatikana kwa tiba ya Ukimwi, vitendo vya ufuska katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam vimeonekana kuongezeka kwa kasi ya ajabu huku joto lake likikadiriwa kufikia nyuzi joto 90, Ijumaa Wikienda lina ripoti kamili.

Uchunguzi uliofanywa mara baada ya kutolewa habari hiyo umebaini kuwa, baadhi ya watu hasa machangudoa wameongeza spidi ya kufanya ngono zembe na wengine kudiriki kusherehekea kufanya hivyo.

Imebainika kuwa kupatikana kwa dawa hiyo kumewafanya hata wale waliokuwa wakiogopa kufa kwa kuhakikisha wanafanya ngono salama, kuingia kwenye hatari hiyo kwa kasi mpya, wakiamini kuwa hata wakiukwaa Ukimwi dawa ipo.


Katika sehemu ya uchunguzi huo,maeneo mbalimbali ya jiji yanayosifika kwa biashara ya uchangudoa na kushuhudia shamra shamra za aina yake zilizohusishwa na upatikanaji wa tiba hiyo ya ngoma.


Miongoni mwa maeneo hayo ni Kinondoni, Oysterbay karibu na Oysterbay Hotel, Manzese Uwanja wa Fisi, Jolly Club na Buguruni ambapo dadapoa hao walionekana kuwa na nyuso za furaha huku baadhi wakipaza sauti kwa kusema: “Dawa ya Ukimwi imepatikana sasa ni kujiuza kwa kwenda mbele na hakuna kutumia kondomu.”


Eneo la Afrika Sana, Sinza, baadhi ya dada poa walioelezwa uwepo wa mkono wa sheria hata kama tiba ya Ukimwi inaelezwa kupatikana, walijibu: “Sheria nsheria nini? Huyo Kova atukome kwanza, kwa sababu kama dawa ya Ukimwi imepatikana tatizo lingine la nini? Atupe uhuru jamani!” 


Katika hali ya kustaajabisha katika eneo la Kinondoni Makaburini, baadhi ya machangudoa walifanya pati ya kusherehekea ujio wa dawa hiyo kwa kunywa pombe na kula nyama choma.


Wakiongea na  katika nyakati tofauti wauza miili hao walisema kuwa, ujio wa dawa hiyo ni mkombozi kwao kwani itawaweka katika nafasi nzuri ya kufanya biashara hiyo kwa kujiachia zaidi tofauti na ilivyokuwa huko nyuma.


Walisema, awali walikuwa wakilazimika kukaribisha majadiliano kati yao na wateja wao kuhusiana na kutumia au kutotumia kondomu ambapo bei zilikuwa zikitofautiana lakini sasa bei itakuwa ni moja tu.

“Kwa kweli taarifa za kupatikana kwa dawa hii tumezipokea kwa furaha sana, hii itatufanya tuwe huru kufanya biashara hii tofauti na huko nyuma ambapo tulikuwa tukitumia kondomu kwa shingo upande, sasa ni full kujiachia,” alisema dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mwanaidi White mkazi wa Buguruni ambaye hufanya biashara hiyo eneo la Kinondoni.

Uchunguzi huo pia imebainika kuwa soko la kondom sasa limeshuka kwa kiasi kikubwa kwani licha ya machangudoa hata baadhi ya wapenzi, wemeanza kutoona sababu ya kutumia kifaa hicho ambacho bado kina umuhimu mkubwa katika kujikinga na VVU.

Katika uchunguzi huo pia, imebainika kuwepo kwa  baadhi ya SMS ambazo baadhi ya watu wanatumiana na nyingine katika mitandao ya intaneti kama barua pepe na facebook.
Ujumbe huo, una maudhui ya kuwataka watu kutojali chochote kwa sababu dawa ya Ukimwi imepatikana.

“Ni zamu yetu kutesa wadau. Ukimwi umesumbua mno akili yetu. Sasa dawa imepatikana, kondomu zinaenda likizo mpaka uje ugonjwa mwingine,” unasomeka ujumbe huo ambao unasambazwa kwa SMS na barua pepe na facebook.

Hata hivyo, wananchi wantahadharishwa kuwa, upatikanaji wa dawa hiyo isiwe sababu ya kujiachia na kujiweka katika mazingira ya kupata maambukizi kwani Ukimwi bado ni ugonjwa hatari.

Inashauriwa watu kuendelea kujali afya zao kwani umakini usipokuwepo, vifo vingi vinaweza kutokea hasa itakapotokea dawa hiyo kuchelewa nchini. Aidha, hata bila Ukimwi, kondomu ni muhimu kwa ajili ya magonjwa mbalimbali ya zinaa.

CREDITS:-GPL

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA HABARI YA MJINI
Copyright © 2011. AROUND THE WORLD - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA HABARI YA MJINI
Proudly powered by Blogger