Wednesday, March 12, 2014

NMB YAWAKOMBOA VIJANA KIUCHUMI KWA KUWAPA MIKOPO NAFUU YA PIKIPIKI

  • Ni mikopo kwa ajili ya pikipiki za miguu miwili na mitatu
Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni tatu yaani Fair Deal Auto Private Ltd inayosambaza pikipiki za miguu miwili na mitatu aina ya Bajaji, kampuni ya Car & General Limited Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya TV’S King pamoja na kampuni ya Quality Motors inayosambaza pikipiki za miguu miwili aina ya Honda wameingia ubia ili kuwawezesha wananchi kupata mikopo nafuu ya kumiliki pikipiki za miguu miwili na mitatu.
Hii yote ni katika kuendeleza azma ya NMB inayolenga kubuni huduma na bidhaa mbalimbali za kibenki zinazogusa kwakaribu mahitaji ya wateja na watanzania kwa ujumla.
three wheeler 1Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt Mary Nagu akikata utepe kama ishara ya ufunguzi rasmi wa uwezeshwaji kwa wateja wa NMB kupitia mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu kutoka benki ya NMB. Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya Tilapia ya jijini Mwanza 
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mikopo hii jijini Mwanza, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mary Nagu amesema “Mikopo hii ya pikipiki itawasaidia sana vijana na wananchi kwa ujumla kuweza kumiliki pikipiki zitakazowawezesha kuendesha maisha yao ya kila siku. Binafsi natambua ajira kwa vijana imekua ni changamoto maeneo mengi nchini hivyo basi ningependa kuwasisitiza vijana wachukue fursa hii inayotolewa na NMB kuweza kumiliki biashara zao wenyewe na kujikimu kiuchumi.”
NAGU 6Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt. Mary Nagu akipeana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Geita Saidi Magalula wakati wa uzinduzi huo.
Vilevile kutoka NMB, Mkuu wa Kitengo cha Biashara za kibenki, Bw. Filbert Mponzi amesema kuwa bidhaa hii mpya inalenga kupunguza changamoto za ajira kwa vijana hapa nchini.
“NMB itaendelea kubuni bidhaa ili kupambana na changamoto za ajira zinazowakumba wateja. Tutaendelea kushirikiana na makampuni kama Fair Deal Auto Private Ltd, Car & General Limited Ltd pamoja na Quality Motors ili kupata bidhaa zenye ubora zaidi.” alisema Mponzi.
NAGU 4
Mkuu wa Kitengo cha Biashara za benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi wakati wa uzinduzi wa mpango wa uwezeshwaji kwa wateja wa NMB kupitia mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu kutoka benki ya NMB. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya ziwa, Bw. Straton Chilongola.
Marejesho ya mkopo huu wa pikipiki ya miguu miwili na mitatu yanatolewa ndani ya muda wa miezi 24, ambapo kwa kipindi hiki chote, mteja ataendelea kurejesha makato yake ya kila mwezi kwakuzingatia taratibu za makubaliano yatakayofanyika baina ya mteja na benki ya NMB.
Mikopo hii pia inawekewa bima kwa ajili ya ulemavu au kifo kitakachomtokea mmliki wa pikipiki iliyochukuliwa mkopo. Bima hii ni kwaajili ya kumpa unafuu mkopaji endapo atapata matatizo ya kiafya ambayo yatamfanya apate ulemavu au kupoteza maisha. 
Mikopo hii yenye masharti nafuu inatolewa kwa mteja yeyote ambaye atatitimiza vigezo vilivyowekwa ili kupata mkopo huu. Anachotakiwa kufanya mteja ni kulipia asilimia thelathini ( 30%) ya bei ya pikipiki ya miguu miwili au mitatu kama inavyouzwa na wasambazaji wa pikipiki hizi za Fair Deal Auto Private Ltd , Car & General Ltd pamoja na Quality Motors.
Kwa maelezo zaidi temmbelea matawi ishirini na moja tu ya NMB nchi nzima yanayotoa mikopo hii kama ifuatavyo: Mwanza-Buzuruga na Kenyata Road,
Dar es Salaam-Tegeta, Magomeni, Mwenge, Mbezi Beach, Temeke,  Ilala, Mlimani City, Msasani na Airport
Arusha-Clock Tower na Arusha Market
Manyara-Babati na Katesh
Dodoma
Mbeya-Mwanjelwa, Mbalizi Road na Usongwe
Moshi-Nelson Mandela na Tanga-Madaraka
NMB BENKI YAKO

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA HABARI YA MJINI
Copyright © 2011. AROUND THE WORLD - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA HABARI YA MJINI
Proudly powered by Blogger