Tuesday, March 11, 2014

MASIKINI...!! NYUMBA YA MSANII WA BONGO MOVIES YATEKETEA KWA MOTO NA KUHARIBU KILA KITU..!!! TAZAMA HAPA


 Ashura Rashid ‘Saladini’.
NYUMBA ya msanii wa filamu za Kibongo aliyewahi kutamba na muvi kali ya Saladini, Ashura Rashid ‘Saladini’ imeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa, huku msanii huyo akihaha kusaka hifadhi kwa majirani, Chande Abdallah anakujuza.
Tukio hilo lilitokea asubuhi ya Machi 6, mwaka huu maeneo ya Bugando jijini Mwanza wakati msanii huyo akiwa kwa majirani zake ambapo chanzo cha moto huo kilidaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Akizungumza na Showbiz kwa njia ya simu, Saladini alisema kuwa kwa sasa analala kwa majirani kwa kuwa kila kitu chake kimeteketea kwa moto.

“Namshukuru Mungu hakuna aliyedhurika lakini nimepata hasara kubwa sana kwani hakuna kitu kilichotoka salama humo ndani,” alisema Saladini kwa masikitiko


gp

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA HABARI YA MJINI
Copyright © 2011. AROUND THE WORLD - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA HABARI YA MJINI
Proudly powered by Blogger