Monday, March 10, 2014

MKASA MZIMA JINSI BABA ALIVYOMCHINJA MWANAYE... HUU HAPA

Stori : Mwandishi Wetu , KAHAMA
MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika Shule
ya Msingi Majengo , Kahama mkoani
Shinyanga, Said Siraji (13 ) anaendelea vizuri
katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama
alikolazwa baada ya kunusurika kifo kwa
kuchinjwa shingoni na baba yake mzazi kwa
madai ya kushindwa kumtibu mtoto huyo kwa
matatizo yake ya afya.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo , Dokta
Joseph Fwoma alisema Said anaendelea vizuri
baada ya kufikishwa hospitalini hapo alfajiri ya
Machi 6, mwaka huu baada kuokotwa na
wasamaria wema akiwa anakimbia huku
akivuja damu shingoni .
Dokta Fwoma alisema walimfanyia upasuaji na
kumshona sehemu ya koromeo aliyochinjwa
na hadi alasiri ya siku hiyo , hali yake ilikuwa
ikiendelea vizuri alipoongezewa damu .
Naye mama mzazi wa Said, Mariamu Idd (35 ),
alisema siku moja kabla ya tukio, baba mzazi
wa mtoto huyo, Siraji Salvatory , 45,
(waliachana) alikwenda kwake Majengo na
kumchukua .
Mama huyo alisema asubuhi iliyofuata
alishtuka sana kupigiwa simu na nduguye
mmoja akielezwa mtoto wake amechinjwa na
aliyehusuka ni baba yake mzazi .
“ Kwa kweli nilishtuka sana , tena sana.
Mwanangu angekufa maana baada ya
kumchinja koromeo baba yake aliamini
ameshammaliza akamwacha porini kisha yeye
akakimbilia Kituo cha Polisi Kahama
kujisalimisha ( hadi sasa anashikiliwa kituoni
hapo).
Mariam alisema, awali Salvatory alikuwa
akimchukua Said na kwenda naye nyumbani
kwake Malunga baada ya siku kadhaa
alimrudisha akidai amechoshwa na gharama
za matibabu kutokana na mtoto huyo kuwa na
matatizo ya kiafya (hakuyasema ).
Jeshi la Polisi wilayani Kahakama
limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA HABARI YA MJINI
Copyright © 2011. AROUND THE WORLD - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA HABARI YA MJINI
Proudly powered by Blogger