Monday, March 10, 2014

Taarifa ya Mahakama kuhusu Kesi ya Msanii AT Kushindwa Kumlipa Mganga wake wa Kienyeji.

Kesi
ya madai iliyofunguliwa mwezi uliopita
na mganga wa jadi dhidi ya AT ambaye
ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, leo
ndo ilikua tarehe yake katika mahamaka
ya mwanzo Buguruni…
Asubuhi AT alifika mahakamani mapema
na ilipofika zamu yake akaitwa na na
kusomewa shitaka na AT alikanusha…
Kesi imeahirishwa mpaka tarehe 04 April
2014, ambapo mdai ambaye ni mganga Dr
sherif ametakiwa kwenda na vielelezo
vyote kuthibitisha madai hayo, kesi hiyo, Dr sherif anadai kuwa
kati ya mwaka 2010 na mwaka 2013
alimtibu msanii AT, na msanii huyo
hakulipa bili  za matibabu  hayo.
Matibabu hayo ni pamoja na kuinua nyota
yake, kumpatia tuzo ya kili mwaka 2013,
na mengineyo .

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA HABARI YA MJINI
Copyright © 2011. AROUND THE WORLD - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA HABARI YA MJINI
Proudly powered by Blogger