Wednesday, March 12, 2014

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA(THBUB) YATOA TAARIFA YAKE YA KIFO CHA DAUDI MWANGOSI

Mwenyekiti wa Tume Ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora Jaji Kiongozi (Mstaafu) Amiri Ramadhan  Manento (katikati) akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani jijini  Dar es Salaam  Oktoba 10,2012 wakati akitoa muhtasari wa  taarifa ya Uchunguzi wa Tume yake kuhusu tukio lililopelekea kifo cha Daudi Mwangosi kilichokea Septemba 2, 2012 kijijini Nyololo. Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa. (Kushoto) ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya  Haki za Binadamu na Utawala Bora Mahfoudha.A. Hamid  na (kulia) ni  Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Tume hiyo Florida Kazora. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Mwenyekiti wa Tume Ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ambae ni Jaji Kiongozi (Msataafu) Amiri Manento (kulia) akitoa muhtasari muhtasari kwa waandishi wa habari hawapo pichani jijini Dar es Salaam Oktoba 10,2012   wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ya Uchunguzi wa tukio lililopelekea kifo cha  mwandishi wa habari wa Chanel Ten Daudi Mwangosi hapo Sept,2,2012 kikijijni Nyololo ,wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. Pichani kulia na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Mahfoudha A.Hamid na kulia ni (kulia) Florida Kazora   (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Baadhi ya wadau na waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo
source: full shangwe blog

Read more >>
widgets for blogger

NMB YAWAKOMBOA VIJANA KIUCHUMI KWA KUWAPA MIKOPO NAFUU YA PIKIPIKI

  • Ni mikopo kwa ajili ya pikipiki za miguu miwili na mitatu
Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni tatu yaani Fair Deal Auto Private Ltd inayosambaza pikipiki za miguu miwili na mitatu aina ya Bajaji, kampuni ya Car & General Limited Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya TV’S King pamoja na kampuni ya Quality Motors inayosambaza pikipiki za miguu miwili aina ya Honda wameingia ubia ili kuwawezesha wananchi kupata mikopo nafuu ya kumiliki pikipiki za miguu miwili na mitatu.
Hii yote ni katika kuendeleza azma ya NMB inayolenga kubuni huduma na bidhaa mbalimbali za kibenki zinazogusa kwakaribu mahitaji ya wateja na watanzania kwa ujumla.
three wheeler 1Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt Mary Nagu akikata utepe kama ishara ya ufunguzi rasmi wa uwezeshwaji kwa wateja wa NMB kupitia mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu kutoka benki ya NMB. Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya Tilapia ya jijini Mwanza 
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mikopo hii jijini Mwanza, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mary Nagu amesema “Mikopo hii ya pikipiki itawasaidia sana vijana na wananchi kwa ujumla kuweza kumiliki pikipiki zitakazowawezesha kuendesha maisha yao ya kila siku. Binafsi natambua ajira kwa vijana imekua ni changamoto maeneo mengi nchini hivyo basi ningependa kuwasisitiza vijana wachukue fursa hii inayotolewa na NMB kuweza kumiliki biashara zao wenyewe na kujikimu kiuchumi.”
NAGU 6Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt. Mary Nagu akipeana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Geita Saidi Magalula wakati wa uzinduzi huo.
Vilevile kutoka NMB, Mkuu wa Kitengo cha Biashara za kibenki, Bw. Filbert Mponzi amesema kuwa bidhaa hii mpya inalenga kupunguza changamoto za ajira kwa vijana hapa nchini.
“NMB itaendelea kubuni bidhaa ili kupambana na changamoto za ajira zinazowakumba wateja. Tutaendelea kushirikiana na makampuni kama Fair Deal Auto Private Ltd, Car & General Limited Ltd pamoja na Quality Motors ili kupata bidhaa zenye ubora zaidi.” alisema Mponzi.
NAGU 4
Mkuu wa Kitengo cha Biashara za benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi wakati wa uzinduzi wa mpango wa uwezeshwaji kwa wateja wa NMB kupitia mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu kutoka benki ya NMB. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya ziwa, Bw. Straton Chilongola.
Marejesho ya mkopo huu wa pikipiki ya miguu miwili na mitatu yanatolewa ndani ya muda wa miezi 24, ambapo kwa kipindi hiki chote, mteja ataendelea kurejesha makato yake ya kila mwezi kwakuzingatia taratibu za makubaliano yatakayofanyika baina ya mteja na benki ya NMB.
Mikopo hii pia inawekewa bima kwa ajili ya ulemavu au kifo kitakachomtokea mmliki wa pikipiki iliyochukuliwa mkopo. Bima hii ni kwaajili ya kumpa unafuu mkopaji endapo atapata matatizo ya kiafya ambayo yatamfanya apate ulemavu au kupoteza maisha. 
Mikopo hii yenye masharti nafuu inatolewa kwa mteja yeyote ambaye atatitimiza vigezo vilivyowekwa ili kupata mkopo huu. Anachotakiwa kufanya mteja ni kulipia asilimia thelathini ( 30%) ya bei ya pikipiki ya miguu miwili au mitatu kama inavyouzwa na wasambazaji wa pikipiki hizi za Fair Deal Auto Private Ltd , Car & General Ltd pamoja na Quality Motors.
Kwa maelezo zaidi temmbelea matawi ishirini na moja tu ya NMB nchi nzima yanayotoa mikopo hii kama ifuatavyo: Mwanza-Buzuruga na Kenyata Road,
Dar es Salaam-Tegeta, Magomeni, Mwenge, Mbezi Beach, Temeke,  Ilala, Mlimani City, Msasani na Airport
Arusha-Clock Tower na Arusha Market
Manyara-Babati na Katesh
Dodoma
Mbeya-Mwanjelwa, Mbalizi Road na Usongwe
Moshi-Nelson Mandela na Tanga-Madaraka
NMB BENKI YAKO
Read more >>

Tuesday, March 11, 2014

MASIKINI...!! NYUMBA YA MSANII WA BONGO MOVIES YATEKETEA KWA MOTO NA KUHARIBU KILA KITU..!!! TAZAMA HAPA


 Ashura Rashid ‘Saladini’.
NYUMBA ya msanii wa filamu za Kibongo aliyewahi kutamba na muvi kali ya Saladini, Ashura Rashid ‘Saladini’ imeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa, huku msanii huyo akihaha kusaka hifadhi kwa majirani, Chande Abdallah anakujuza.
Tukio hilo lilitokea asubuhi ya Machi 6, mwaka huu maeneo ya Bugando jijini Mwanza wakati msanii huyo akiwa kwa majirani zake ambapo chanzo cha moto huo kilidaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Akizungumza na Showbiz kwa njia ya simu, Saladini alisema kuwa kwa sasa analala kwa majirani kwa kuwa kila kitu chake kimeteketea kwa moto.

“Namshukuru Mungu hakuna aliyedhurika lakini nimepata hasara kubwa sana kwani hakuna kitu kilichotoka salama humo ndani,” alisema Saladini kwa masikitiko


gp
Read more >>

AIBUU....MKE WA MTU AFUMANIWA AKINGONOKA NA KIDUME CHUMBANI KWA MUMEWE

Timbwili I zito limeibuka baada ya mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Samora kumnasa ‘live’ mkewe Hadija akimsaliti kwa kuvunja amri ya sita na hawara ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tena kwenye chumba chao..

Habari kutoka chanzo cha uhakika kilitonya kuwa Samora na Hadija ni wanandoa waliooana Bomani pale Magomeni, Dar, mwaka 2009 na katika ndoa yao wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume.
Tukio hilo la fumanizi lilijiri maeneo ya Kinondoni-Kwamsisiri, Dar nyumbani kwa wanandoa hao, majira ya saa 1:00 usiku, Julai 29, mwaka huu.

Habari zilieleza kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, ndoa ya wawili hao ilitumbukia nyongo na kuingia kwenye mgogoro ambapo pamoja na kuweka mambo sawa, waliendelea kukwaruzana mara kwa mara.

Ilidaiwa kuwa chanzo cha wawili hao kuhitilafiana ni kutokana na mwanaume kumtuhumu mkewe kutoa tunda nje ya ndoa.

Ikasemekana kuwa baadaye wapambe walimfuata Samora na kumtonya kuwa mkewe amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na kidume mwingine nje ya ndoa yao ndiyo maana amekuwa akimletea nyodo .

Iliendelea kudaiwa kuwa baada ya ndoa kutibuka, Samora alikuwa mnyonge na mwenye msongo wa mawazo hivyo ikabidi aikimbie nyumba kwa muda na kwenda kwa wazazi wake.

Ilisemekana kuwa, Samora alirejea nyumbani huku akifanya uchunguzi wa nguvu akiwatumia majirani kumpatia taarifa kuhusu kila mwanaume aliyeingia na kutoka nyumbani kwake yeye akiwa hayupo.
Uchunguzi wa Samora ulibaini kuwa, Hadija alikuwa ‘akibanjuka’ nje ya ndoa na mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Rwekaza ambaye ni mfanyakazi serikalini.

Habari za kina zilisema kuwa, Samora alitonywa kwamba jamaa alikuwa akitimba na gari aina ya Suzuki Swift 1.3 na siku nyingine alikuwa akilala hadi asubuhi bila tone la soni kuwa Hadija ni mke wa mtu.


Baada ya kupata uhakika huo ndipo Samora akajipanga kwa kuwatafuta vijana wa mtaani ili Rwekaza atakapofika nyumbani hapo kulala na mkewe wamvamie na kumfanyizia.

Bila kufahamu kuwa anasubiriwa kwa hamu majira yaa saa 1:00 usiku, Rwekaza huyooo, akatinga nyumbani hapo na moja kwa moja akafikia chumbani kama kawaida yake.

Wakiwa chumbani, ilidaiwa kuwa waliendelea na mambo yao huku Rwekaza akiwa tumbo wazi na suruali yake amefungua zipu huku Hadija akiwa amesaula na kubaki na ‘kufuli’, kisha akajifunga khanga moja.


Katika fumanizi hilo, Samora alitinga chumbani humo akiwa ameambatana na kundi la vijana kibao ambao walikuwa na lengo moja tu, kumfanyia kitu mbaya Rwekaza.


Wakiwa chumbani, kuliibuka bonge la timbwili baada ya Samora kumshuhudia mwenza wake aliyekula kiapo cha kutotengana naye akisaliti ‘laivu’ penzi lao.

Baada ya kuona machafuko makubwa ya hali ya hewa chumbani, mwanahabari wetu aliwataarifa polisi katika Kituo cha Kwamsisiri ambao walifika maeneo hayo na kufanya kazi kubwa na nzuri ya kuepusha balaa au mauaji kwa kuwa Samora alikuwa na hasira kali.



Ili kuthibitisha kuwa ni mkewe wa ndoa, Samora alizama kabatini na kuchomoa cheti cha ndoa na picha walizopiga siku ya ndoa yao zikiwaonesha wakiwa na tabasamu la ‘mimi na wewe milele’ kabla ya shetani ‘kufanya yake’ kwenye unganiko lao.


Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo liliwasikitisha wengi huku wakiamini kabisa kuwa ni nadra matukio ya mafumanizi kutokea katika kipindi cha mfungo.

“Jamani hata Mwezi Mtukufu? Ni aibu sana kwa mke kuingiza mwanaume mwingine kwenye chumba cha mumewe. Kweli hili fumanizi ni kiboko,” alisikika mmoja wa majirani hao walioshuhudia tukio hilo muda mfupi baada ya kufuturu.Source: Global publisher
Read more >>

POMBE SI CHAI: TAZAMA PICHA 6 ZA AIBU:NGUVU YA POMBE YAMUADHILISHA MISS HUYU










Read more >>

STORI YA WABUNGE WA ZIMBABWE KUGOMA KUTAHIRIWA HII HAPA ISOME

 
Wabunge wanaume nchini Zimbabwe wameonekana kutokukubaliana na wito wa kutaka kutahiriwa ili kuonyesha mfano katika kupambana dhidi ya ukimwi, BBC imegundua.
Naibu waziri mkuu Bi Thokozani Khupe alitoa wito huo, kufuatia ushahidi kuwa wanaume waliotahiriwa wana uwezekano wa kuathirika na virusi vya HIV kwa chini ya asilimia 60.
Miongoni mwa wabunge wanane waliozungumza na BBC, mmoja tu alisema atatilia maanani pendekezo lake.
Mmoja aliita hatua hiyo “wazimu”, wakati mwengine alisema ataonyesha mfano mzuri kutokana na tabia yake.
Zimbabwe ni moja ya nchi zilioathirika sana na ugonjwa wa ukimwi na mwaka jana serikali ilizindua kampeni ya kuwatahiri mpaka aslimia 80 ya vijana wa kiume- ambao ni takriban watu milioni tatu.
Shirika la Afya Duniani WHO linawashawishi wanaume kutahiriwa kufuatia utafiti uliofanywa katika nchi nyingine za Afrika.
Hata hivyo, wataalamu wa ugonjwa huo, wanaonya kutumia kondom, kujizuia kufanya ngono au kuwa mwaminifu kwa
SOMA HII: BAADA YA POMBE KUMKOLEA MKE WA MTU AAMUA KUPIGA PICHA ZA UTUPU GEST AKIVUNJA AMRI YA SITA NA KIDUME. mwenza mmoja ni miongoni mwa njia bora zaidi katika kujikinga dhidi ya virusi vya ukimwi.
Source: BBC SWAHILI.
Read more >>

HII NI KWA WANAUME MNAOPENDA KUZAMA CHUNVINI (NGONO YA MDOMO), SOMA HAPA MADHARA YAKE



Namna mdomo unavyoharibika kutokana na ngono kufanywa kwa kutumia mdomo. Picha ya Maktaba. 
Na Hadija Jumanne, Mwananchi
  • Baadhi ya watu ambao wanakumbwa na ugonjwa huu shingo huvimba kama hivi. Hata hivyo wapo wenye kuvimba hivi lakini si kwa sababu walifanya ngono kwa kutumia mdomo, isipokuwa yaweza kuwa ni sababu nyingine zikiwemo kurithi. 
  • Wataalamu wa masuala ya afya wanashauri kwamba ni muhimu sana watu wakaachana kabisa na tabia hii kutokana na ukweli kwamba siyo tu kwamba ni hatari kwa afya, pia ni sawa na kujiua mwenyewe, kwani kitendo hicho kinachangia magonjwa mengi.
BOFYA HAPA: TAZAMA PICHA ZA WEMA SEPETU ZILIZOWATOA UDENDA MIDUME KIBAO
Leo ni siku ya Saratani Duniani. Wakati tunaadhimisha siku hii hapa nchini idadi ya vijana ambao ni tegemeo la taifa inazidi kupungua kutokana kuangamia kwa saratani ikiwemo ya koo.
Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya saratani ya koo husababishwa na ngono ya mdomo maarufu kama ‘Oral Sex”.
Utafiti huo unaonyesha saratani ya koo licha ya kuambukizwa na njia mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye pilipili,
 pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.
Utafiti unaonyesha watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya kufanya ngono wakitumia midomo hasa  ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.
Katika utafiti  huo wa hivi karibuni, ulibaini wanaume 747  na wanawake wakiwa 472 hugundulika kila mwaka kuwa na saratani hiyo huku wanaopoteza maisha kila mwaka ni wanaume 444 wakifuatiwa na wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo.
Utafiti unabainisha kuwa asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45 wanatumia staili ya kuwanyonya wenza wao sehemu za siri lengo likiwa ni  kuwavutia wapenzi wao katika  kushiriki ngono.
Vijana  wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa sasa kutokana na ugonjwa huo kuonekana kuwaathiri kwa kasi, huku wengi wakiwa hawajui athari zake. Baadhi hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe wanajitafutia kifo kwa kufanya vitendo hivyo.
Utafiti unaonyesha kwa watu wazima walio wengi hawana muda wa kufanya hayo wanayofanya vijana, hivyo kujikuta angalau wanakuwa salama na kupatwa na saratani ya koo kwa njia hiyo inayoonekana kama ni chafu pia.
Daktari  Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa anasema saratani ya  koo ni  ya pili katika mtiririko wa saratani zinazowapata wanaume  nchini, ikiongozwa na ile ya  ngozi (Karposi’s Sarcoma) ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kuna saratani aina zaidi ya 24 zinazoisumbua Tanzania.
Anasema mbali na staili hiyo pia, kuna baadhi ya watu hupata saratani ya  koo kwa kurithi kutoka kwa wazazi wao na wengine kuwa na  umri mkubwa ambao huchangia kupata tatizo hilo, lakini siyo kwa asilimia kubwa kama ile ya ngono ya mgomo.
“Hali hii ya vijana wenye umri huo kuwanyonya wanawake inatokana na ujana, wengine wanaiga kwenye mitandao, lakini mambo haya hayakuwepo zamani tofauti na sasa, utakuta wanaume
http://mtukwaotz.blogspot.com/2014/03/picha-zaidifull-mitego-ya-mrembo-wa.html ili aweze  kumvutia mwanamke anamfanyia hivyo sehemu za siri, lakini zamani staili hii haikuwepo kabisa,” 
BOFYA HAPA: PICHAZ 5 KALI ZA KIMAHABA...VANESSA MDEE KITOVU NJE FULL MITEGO AISEE.... anasema  Dk Kahesa na kuongeza.
source: mwananchi
Read more >>
 
Support : KARIBU TENA HABARI YA MJINI
Copyright © 2011. AROUND THE WORLD - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA HABARI YA MJINI
Proudly powered by Blogger