Monday, March 10, 2014

PPF KUWABANA WAAJIRI WASIOWALIPIA WAFANYAKAZI

Meneja Huduma kwa Wateja na Wanachama
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bw . Godfrey
Mollel akieleza jambo kwa waandishi wa
habari ( hawapo pichani ) .
Stori : Mwandishi Wetu
MFUKO wa Pensheni (PPF ) umesema kwamba
endapo waajiri wa sekta mbalimbali
waliojiunga na mfuko huo watashindwa
kuwakilisha michango ya wafanyakazi wao
kwa muda unaotakiwa hawatasita
kuwachukulia hatua.
Kauli hiyo ilitolewa na Meneja Huduma kwa
Wanachama wa PPF , Godfrey Mollel wakati
alipokuwa akitoa mada juu ya kujiunga na
mfuko huo na faida zake katika mkutano wa
mwaka wa waandishi na wadau wa habari
uliofanyika wiki iliyopita katika Ukumbi wa
Karimjee jiini Dar es Salam .
Meneja huyo alifafanua kuwa kuna baadhi ya
waajiri ambao wafanyazi wao ni wanachama
lakini wamekuwa wakichelewa kuwakilisha
michango ya wafanyakazi wao.
“ Tutakuwa tunawakumbusha kwanza bila
kuwachukulia hatua lakini pale
inaposhindikana ndipo tutafikia hatua hiyo ya
kuangalia njia nyingine ikiwa ni pamoja na
kuwafikisha mahakamani , ” akisema Mollel .
Hata hivyo , amewataka waajiri ambao bado
hawajajiunga, wajiunge pamoja na wafanyakazi
wao au mjasiriamali nao wanaweza kujiunga
na mfuko huo .
Awali mkutano huo ulifunguliwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa PPF , William Erio
(pichani ) na ulihudhuriwa na waandishi na
wadau wa habari 130 ambapo watu 90
walijiunga na mfuko huo siku ya tukio.

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA HABARI YA MJINI
Copyright © 2011. AROUND THE WORLD - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA HABARI YA MJINI
Proudly powered by Blogger