- Ni mikopo kwa ajili ya pikipiki za miguu miwili na mitatu
Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni tatu yaani Fair Deal
Auto Private Ltd inayosambaza pikipiki za miguu miwili na mitatu aina
ya Bajaji, kampuni ya Car & General Limited Ltd inayosambaza
pikipiki za miguu mitatu aina ya TV’S King pamoja na kampuni ya Quality
Motors inayosambaza pikipiki za miguu miwili aina ya Honda wameingia
ubia ili kuwawezesha wananchi kupata mikopo nafuu ya kumiliki pikipiki
za miguu miwili na mitatu.
Hii
yote ni katika kuendeleza azma ya NMB inayolenga kubuni huduma na bidhaa
mbalimbali za kibenki zinazogusa kwakaribu mahitaji ya wateja na
watanzania kwa ujumla.
Waziri
wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt Mary
Nagu akikata utepe kama ishara ya ufunguzi rasmi wa uwezeshwaji kwa
wateja wa NMB kupitia mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu kutoka benki ya NMB. Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya Tilapia ya jijini Mwanza
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa mikopo hii jijini Mwanza, Waziri wa
Uwezeshaji na Uwekezaji kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mary Nagu amesema “Mikopo
hii ya pikipiki itawasaidia sana vijana na wananchi kwa ujumla kuweza
kumiliki pikipiki zitakazowawezesha kuendesha maisha yao ya kila siku.
Binafsi natambua ajira kwa vijana imekua ni changamoto maeneo mengi
nchini hivyo basi ningependa kuwasisitiza vijana wachukue fursa hii
inayotolewa na NMB kuweza kumiliki biashara zao wenyewe na kujikimu
kiuchumi.”
Waziri
wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Mhe. Dkt. Mary
Nagu akipeana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Geita Saidi Magalula wakati wa
uzinduzi huo.
Vilevile kutoka NMB, Mkuu wa Kitengo cha Biashara za kibenki, Bw. Filbert Mponzi amesema kuwa bidhaa hii mpya inalenga kupunguza changamoto za ajira kwa vijana hapa nchini.
“NMB
itaendelea kubuni bidhaa ili kupambana na changamoto za ajira
zinazowakumba wateja. Tutaendelea kushirikiana na makampuni kama Fair Deal Auto Private Ltd, Car & General Limited Ltd pamoja na Quality Motors ili kupata bidhaa zenye ubora zaidi.” alisema Mponzi.
Mkuu
wa Kitengo cha Biashara za benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi wakati wa
uzinduzi wa mpango wa uwezeshwaji kwa wateja wa NMB kupitia mikopo ya pikipiki za miguu miwili na mitatu kutoka benki ya NMB. Kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya ziwa, Bw. Straton Chilongola.
Marejesho
ya mkopo huu wa pikipiki ya miguu miwili na mitatu yanatolewa ndani ya
muda wa miezi 24, ambapo kwa kipindi hiki chote, mteja ataendelea
kurejesha makato yake ya kila mwezi kwakuzingatia taratibu za
makubaliano yatakayofanyika baina ya mteja na benki ya NMB.
Mikopo
hii pia inawekewa bima kwa ajili ya ulemavu au kifo kitakachomtokea
mmliki wa pikipiki iliyochukuliwa mkopo. Bima hii ni kwaajili ya kumpa
unafuu mkopaji endapo atapata matatizo ya kiafya ambayo yatamfanya apate
ulemavu au kupoteza maisha.
Mikopo
hii yenye masharti nafuu inatolewa kwa mteja yeyote ambaye atatitimiza
vigezo vilivyowekwa ili kupata mkopo huu. Anachotakiwa kufanya mteja ni
kulipia asilimia thelathini ( 30%) ya bei ya pikipiki ya miguu miwili au
mitatu kama inavyouzwa na wasambazaji wa pikipiki hizi za Fair Deal
Auto Private Ltd , Car & General Ltd pamoja na Quality Motors.
Kwa
maelezo zaidi temmbelea matawi ishirini na moja tu ya NMB nchi nzima
yanayotoa mikopo hii kama ifuatavyo: Mwanza-Buzuruga na Kenyata Road,
Dar es Salaam-Tegeta, Magomeni, Mwenge, Mbezi Beach, Temeke, Ilala, Mlimani City, Msasani na Airport
Arusha-Clock Tower na Arusha Market
Manyara-Babati na Katesh
Dodoma
Mbeya-Mwanjelwa, Mbalizi Road na Usongwe
Moshi-Nelson Mandela na Tanga-Madaraka
NMB BENKI YAKO
No comments:
Post a Comment