Ashura Rashid ‘Saladini’.
NYUMBA ya msanii wa filamu za Kibongo aliyewahi kutamba na muvi kali
ya Saladini, Ashura Rashid ‘Saladini’ imeteketea kwa moto na kusababisha
hasara kubwa, huku msanii huyo akihaha kusaka hifadhi kwa majirani,
Chande Abdallah anakujuza.Tukio hilo lilitokea asubuhi ya Machi 6, mwaka huu maeneo ya Bugando jijini Mwanza wakati msanii huyo akiwa kwa majirani zake ambapo chanzo cha moto huo kilidaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Akizungumza na Showbiz kwa njia ya simu, Saladini alisema kuwa kwa sasa analala kwa majirani kwa kuwa kila kitu chake kimeteketea kwa moto.
“Namshukuru Mungu hakuna aliyedhurika lakini nimepata hasara kubwa sana kwani hakuna kitu kilichotoka salama humo ndani,” alisema Saladini kwa masikitiko
gp
No comments:
Post a Comment