Wednesday, March 5, 2014

MDOGO WA KANUMBA AZUA MAPYA, ADAI MAREHEMU KANUMBA ANAMTOKEA MARAKWA MARA SOMA HAPA ALICHOKISEMA

Joseph Shaluwa na Erick Evarist
SETH Bosco aliye mdogo wa marehemu Steven Kanumba, aliyekuwa staa wa filamu za Kibongo, ameibuka na kueleza mambo ya kushangaza, akidai kaka yake huyo amekuwa akimtokea ndotoni.

Marehemu Steven Kanumba.
Seth ndiye msimamizi na mwendeshaji wa Kampuni ya Kanumba The Great Film baada ya kifo cha Kanumba kilichotokea Aprili 07,2012 nyumbani kwake, Sinza – Vatican, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari hizi, wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, kwa sauti ya huzuni, Seth alisema: “Kiukweli sina amani, hii hali inanitesa sana. Kila mara ananitokea ndotoni na kunieleza mambo yanayofanana.”
MAMBO GANI?
“Analalamika kwa nini eti ofisi yake aliyoiacha haina mafanikio. Sasa nashindwa kuelewa, ni mafanikio gani anayozungumzia. Analalamika kwa nini filamu hazitolewi, ni jambo la kweli lakini lipo nje ya uwezo wangu,” alisema Seth.

Seth Bosco.
AMANI: Anakutokea kivipi yaani?
SETH: Nikiwa usingizini, nakuwa kama naota, lakini mazungumzo yanakuwa ya moja kwa moja... ndoto ikikatika, nashtuka na kujikuta nahema kwa kasi.

AMEMTOKEA MARA NGAPI?
“Mara ya tatu sasa, ndiyo maana nimeshindwa kuvumilia. Kinachonishangaza ni kwamba, kila anaponitokea, lazima nishtuke mwishoni na lazima niheme kwa kasi na kutoka jasho jingi.
“Mwanzoni nilichukulia kawaida, lakini alivyonijia mara ya pili na ya tatu nikaona hili suala siyo la kulikalia kimya, ikabidi nimwambie mama.”

MAMA KANUMBA ANASEMAJE?
“Mama alishtuka na ameshangazwa sana na hali hiyo. Ameniuliza imenitokea mara ngapi, nikamwambia tatu, akasema lazima tufanye maombi kuondoa hali hiyo,” alisema Seth huku akionesha uso wa wasiwasi.

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA HABARI YA MJINI
Copyright © 2011. AROUND THE WORLD - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA HABARI YA MJINI
Proudly powered by Blogger