Wednesday, March 5, 2014

LINA AONYESHA WAZI ALIKUA AKIMUHONGOPEA KIMAPENZI AMINI....

Esterlina Sanga ‘Linah’.
Na  Mayasa Mariwata
MWANADADA mwenye sauti tamu kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Esterlina Sanga ‘Linah’ amesema katika maisha yake kamwe hafikirii kuja kuolewa na mwanaume mfupi kwani siyo sampuli yake.

Akipiga stori na paparazi wetu juzikati, Linah alisema atakuwa si mkweli akitamka ana mwanaume mfupi kwani hata jamii itamcheka kwa kuwa hata Amini Mwinyimkuu aliyewahi kuwa mpenzi wake ni mfupi.
“Nisiongee uongo kusema eti sipendi kutoka kimapenzi na mwanaume mfupi wakati nilishawahi kufanya hivyo na siwezi kujiapiza katika hilo, ila kwenye swala la ndoa lazima nizingatie kigezo changu  muhimu cha kuolewa na mwanaume mrefu,” alisema Linah.

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA HABARI YA MJINI
Copyright © 2011. AROUND THE WORLD - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA HABARI YA MJINI
Proudly powered by Blogger