Stori: Joseph Shaluwa
IMEBUMBURUKA! Kumbe staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma, aliye mama wa watoto watatu, mmoja kati yao, alizaa na mkongwe katika Bongo Hip Hop, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’.
Habari kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika kilipasha kuwa Wastara amekaa na siri hiyo moyoni kwa muda mrefu sana.
“Mtoto mmoja alizaa na Solo,
wakati ule Solo akiwa anatamba na nyimbo zake kama Homa ya Dunia, Mambo
ya Pwani na Mtazamo ambao alishirikiana na Afande Sele na Profesa Jay.
Tena leo (juzi Jumatano) ameandika kwenye Instagram na ameweka na picha
ya Solo,” alipasha shosti huyo.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZA LULU NA VAN VICKER WA NIGERIA WAKIWA KATIKA POZI TATA
Haraka paparazi wetu, akazama kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram
na kufanikiwa kuona picha hiyo iliyosindikizwa na maneno: “Baba wa baby
wa miye, Msafiri Kondo a.k.a Solo Thang, moyo wako haukupishana sana na
wa Sajuki (Juma Kilowoko).
“Sijawahi kuyasema haya lakini utazipata salamu huko ulipo. Maisha
yametutenganisha ila sijawahi kugombana na wewe wala familia yako.
Nashukuru kwa upendo wenu juu yangu hasa mama yako. Nawapenda sana na
hata mtoto wenu anawapenda. Dunia ni njia tu, hatujui nani atatangulia.
Nakutakia mafanikio. Inshallah.”
Risasi Jumamosi lilimpandia hewani Wastara ili kupata ufafanuzi juu
ya ishu hiyo ambapo alikuja juu: “Hivi kwa nini mnanifuatafuata sana
jamani? Sasa umesema umeona Instagram, kwa hiyo nikusaidie nini?”
RISASI JUMAMOSI:
Nataka kujua machache kuhusu Solo na huyo mwanaye. Mlianza lini
uhusiano na kwa nini ulikaa kimya kwa muda mrefu. Ni muhimu ufafanue
hili Wastara, maana umeweka kwenye mtandao wa kijamii na wengi wameona.
WASTARA:
Naomba mniache, nina mambo mengi yananisumbua kichwani mwangu. Kama
wameona, acha waone. (Tiiii...tiii...tiiii.... Wastara alikata simu).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment