Tuesday, March 4, 2014

SIKU CHACHE BAADA YA KUSAINI SHERIA KWA MASHOGA NA WASAGAJI, MTOTO WA RAIS MUSEVEN AKIRI KUWA NI MSAGAJI

Katika hali iliyowashangaza wengi mtoto wa kike wa Rais wa Uganda, Yoweri ­Museveni, amekiri ya kuwa yeye ni msagaji alipokuwa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha radio kilichopo Mbarara, Magharibi ya Uganda, huku akisisitiza kwa kusema kuwa anapinga muswada mpya uliopitishwa wa kupinga mapenzi ya jinsia moja ambao imesainiwa hivi karibuni na kuufanya kuwa sheria na baba yake mzazi.

Diana Kamuntu, mtoto wa kike wa Rais Museveni alisema anampenda baba yake katika hali ya kawaidia, ila hakubaliani na Serikali yake juu ya msimamo wake juu ya mapenzi ya jinsia moja, na atapigana juu ya hilo.

    Kwenye maneno aliyosema mtoto huyo wa Rais: “Mimi ni msagaji, ninafanya mapenzi ya jinsia moja. Nimelijua hilo toka nilivyokuwa msichana mdogo. Pia, nimekuwa ni Mkristo kwa miaka yangu yote, ila sitounga mkono sheria yoyote itakayopitishwa na nchi hii ya demokrasia, ambayo itajenga chuki kwa mtu yeyote kisa kwa sababu ya hali yake ya kijinsia itakavyokuwa.

    “Sasa kwa sababu nishaifahamu hali yangu ya kijinsia, najiweka mbele dhidi ya sheria hii mpya na nitawafanya watu wetu waamue juu ya mimi,” alisema kwa hisia kali.


Kwa mujibu wa CodeWit, mahojiano hayo ya mtoto wa Rais yalileta mkanganyiko ndani ya studio na kipindi hicho kilichokuwa kikirusha moja kwa moja (live) ilibidi kisitishwe kabla ya muda.

SWALI: Je Rais Yoweri ­Museveni atamtupa mtoto wake gerezani kwa sababu ni msagaji? Dunia inaangalia...

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA HABARI YA MJINI
Copyright © 2011. AROUND THE WORLD - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA HABARI YA MJINI
Proudly powered by Blogger