MWALIMU Mkuu wa Shule ya
Msingi Rutamba, Wilaya ya Lindi amekutwa akiwa na nguo za ndani pekee
katika usingizi mzito kwenye kibao cha shule hiyo huku akiwa hajitambui
kwa madai ya kilichomkutana kinahusishwa na imani za kishirikina.
Tukio hilo limetokea juzi usiku baada ya mkazi
mmoja wa kijiji hicho, Juma Mbilemoto kumkuta mwalimu huyo akiwa kwenye
kibao hicho wakati alipokuwa anamsindikiza nduguye,Aisha Mbilimoto
aliyekuwa anasafiri kuelekea Dar es Salaam.
Akizungumzia tukio hilo, shuhuda huyo alisema
alimkuta mwalimu huyo akiwa amelala chini ya kibao cha shule akiwa na
nguo ya ndani tu (chupi)huku akikoroma kutokana na kuwa na usingizi
mzito.Alisema awali hakumtambua mtu huyo lakini baada ya kumkaribia
alimtambua kuwa alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na ndipo alipochukua
jukumu la kumwamsha ili amvalishe kanga, lakini aliikataa na kuondoka
kwenda nyumbani kwake akiwa kama alivyokutwa
Kwa upande wao walimu wa shule hiyo walisema kuwa,
wamekosa molari wa kufanya kazi kutokana na kitendo alichofanyiwa
mwalimu mwenzao.
Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, Francis
Milanzi alisema walimu shuleni hapo wamekosa amani na kuwasababishia
kuzihama nyumba zao kwa muda na badala yake kwenda kukesha kwenye
ofisi za walimu tangu tukio hilo litokee.
Ofisa elimu wa Wilaya ya Lindi, Cosmas Magigi
alisema amepokea taarifa za tukio hilo kwa huzuni na amewaomba walimu
kuwa na subira wakati utaratibu wanalishughulikia suala hilo.
Magigi aliongeza kuwa ofisi yake itafanya
utaratibu wa BOFYA HAPA: KUTANA NA MREMBO MWANACHUO MWENYE KALIO LA AJA AMBAYE, WATU WANAHISI ANALITUMIA KUFAHURU MITIHANI kumhamisha mwalimu huyo na kumtafutia shule nyingine huku
akiwataka wakazi wa eneo hilo kujenga ushirikiano na watumishi ili
waweze kutekeleza majukumu yao.
Hili ni tukio la pili kutokea katika halmashauri
hiyo mwaka huu ambapo la kwanza lilitokea April katika Shule ya
Sekondari Ruhokwe, mwalimu wa shule hiyo alilazwa kwenye kibao cha
SOMA HII shule akiwa uchi wa mnyama.
SOMA HII shule akiwa uchi wa mnyama.
No comments:
Post a Comment