Friday, March 7, 2014

MASKINI SHABIKI HUYU WA LIVERPOOL ADUNGWA VISU NA MWENZAKE WA TIMU PINZANI



Liverpool waliishinda Arsenal mabao 5-1 katika mechi yao 
Mwanamume raia wa Kenya anayeshabikia klabu ya soka ya Uingereza ya Liverpool amedungwa kisu na mwenzake wa klabu ya Arsenal na kufariki dunia katika eneo la Meru Mashariki mwa Kenya.
Kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo wawili hao walianza malumbano baada ya mechi kati ya vilabu hivyo kumalizika hapo Jumamosi.
Wawili hao walikua katika baa moja iliyojaa mashabiki wa timu hizo mbili.
Shabiki wa Arsenal anayefanya kazi ya Boda Boda alijawa na hasira baada ya timu yake kukemewa na shabiki wa Liverpool kiasi cha kumdunga mwenzake kisu mara kadhaa, kabla ya kutoweka.
Watu waliokua karibu na eneo la tukio hilo walimsaidia mwathiriwa aliyetambuliwa kama Anthony Muteithia na kumpeleka katika hospitali kuu ya Meru ambapo alifariki dunia wakati akipokea matibabu.
Mkuu wa polisi eneo la Meru Tom Odero amesema wanamsaka shabiki huyo wa Arsenal ambaye amekwenda mafichoni.
Hapo Disemba mwaka jana shabiki wa klabu ya Manchester United nchini Kenya kwa jina Jimmy Macharia alijiua baada ya klabu hiyo kuendelea kuorodhesha matokeo mabaya.
Na mnamo mwaka 2012 Suleiman Alfonso Omondi shabiki wa Arsenal alijitia kitanzi baada ya timu hiyo kushindwa kwenye mechi. Ligi ya Premia nchini Uingereza huvutia ushabiki mkubwa 
bofya hapa kuona majina ya makahaba yaliyotajwa na jeshi la polisi 
nchini Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA HABARI YA MJINI
Copyright © 2011. AROUND THE WORLD - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA HABARI YA MJINI
Proudly powered by Blogger