Thursday, March 6, 2014

MAIMARTHA WA JESE ATIWA MBARONI

Gladness Mallya
Mtangazaji maarufu wa Runinga Bongo, Maimartha Jesse amejikuta akiwekwa nyuma ya nondo kwa madai ya kumtapeli dada mmoja aliyetambulika kwa jina la Zai, mkazi wa Zanzibar.
Maimartha Jesse.
Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa, mtangazaji huyo alilipwa pesa ya kianzio cha shughuli ya u-MC visiwani humo mwezi mmoja uliopita lakini akashindwa kwenda bila sababu za msingi.
“Kifupi Maimartha alifanya usanii, alimzungusha yule dada,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya siku ya tukio kupita na Maimartha kuingia mitini, chanzo hicho kilisema Machi 4, mwaka huu, Zai alimfungia safari hadi Dar na kumpeleka Kituo cha Polisi Oysterbay kabla ya kumalizana.
Alipotafutwa Maimartha kuzungumzia juu ya sakata hilo, alitiririka: “Imeniuma sana, kiukweli alinipa fedha za kianzio huyo dada (Zai) lakini nilishindwa kwa sababu nilipata dharura, hata hivyo nimeshangaa amekwenda kupandisha dau kule polisi tofauti na fedha ndogo aliyonipa, sitaki kuongelea sana lakini nashukuru yameisha.”

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA HABARI YA MJINI
Copyright © 2011. AROUND THE WORLD - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA HABARI YA MJINI
Proudly powered by Blogger