Stori: Mwandishi Wetu
MSANII wa filamu za Kibongo, Kimlola Kimlola ‘Nelly Kim’ amesema anajivunia sana kufanya sinema nyingi na marehemu StevenKanumba na kwamba amejipanga kufuata nyayo zake ili aweze kufanikiwa kwa kutumia kipaji chake.
Akizungumza na Stori Mix, Nelly Kim alisema: “Nafurahi kufanya kazi na marehemu Kanumba. Nimecheza naye zaidi ya sinema 20 pale kwa Mtitu Game.
Nimejifunza kujiongoza na kuamini katika mambo makubwa, ndiyo maana sasa hivi nasimama na kampuni yangu ya Kasinge Production ambayo inatayarisha na kusambaza filamu.
“Nimesharekodi filamu ya kwanza inayoitwa The Word of God ambayo nimecheza na Kajala, Ben, Kambi na wengineo.
Unajua wasanii hatujitambui, tunakubali kunyonywa wakati tunaweza kujitutumua na kusimamia kazi zetu wenyewe. Hiyo ndiyo siri ya mafanikio ya Kanumba ambayo nataka kuitumia ili kufaidika kwenye sanaa.”

No comments:
Post a Comment