Wednesday, March 5, 2014

TAPELI SUGU LA KIZUNGU LAKAMATWA...!! TAZAMA PICHA NA STORI YA TAPELI HUYO WA KIZUNGU...!!


 Hapa akitia huruma
Yule mzungu aliyekuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kutuhuma za kuwatapeli wananchi kwa Euro Feki hatimae amekamtwa kikomandoo akijaribu kununua gari kwa pesa hizo feki. 
 
Habari za uhakika zilizotua mezani zilisema mzungu huyo ambae ni Raia wa South Africa aliyeahamika kwa jina la  JAN ELOFF oambae anaishi maeneo ya Msasani Jijini Dar.
Kwa mujibu wa taarifa zilizonaswa na mtandao huu hatari kwa habari za uchunguzi zilisema mzungu huyo ambae alikuwa anatuhumiwa kumpiga zaidi ya Euro hizo feki 700 mwandishi mwandamizi wa blog hii na DTV Bw. Livingstone Mkoi mwanzoni mwa januari mwaka huu kisha kufungua kituo cha polisi Oysterbay nakupatia kumbukumbu hii OB/RB/ 2972/14 KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU,pamoja na Kutoa Euro Feki.
 
Baada ya tukio hilo la kutapeliwa mwanahabari huyo Jeshi la Polisi lilitangaza msako mkali wa kumtafuta mzungu huyo ambae alikuwa akishirikiana na wadada wawili ambao ni araia wa Cameroon na Nigeria pamoja na mwanaume wa kitanzania ambao baada ya tukio la kukatwa mwenzao wanaendelea kutafutwa usiku na mchana na tayari ameshawataja wenzake anaoshirikiana nao.
Kufuatia kukamatwa kwa mzungu huyo wananchi wengi wamempongeza Kamanda Kova kwa kufanikisha kukamatwa mzungu huyo.

Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni limetoa rai kwa mtu yeyote ambae amewahi kupigwa na mzungu huyo basi wafike haaka kituo cha polisi Oysterbay kwa ajili ya kumtambua mzungu huyo.

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA HABARI YA MJINI
Copyright © 2011. AROUND THE WORLD - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA HABARI YA MJINI
Proudly powered by Blogger