Jiji la dar es
salaam huwa ni tamu lakini lina kero zake na uenda kero ni nyingi kuliko raha
zilizopo… moja wapo ya kero kubwa zaidi ni hili ambalo bila shaka kila mmoja
wetu anayeishi uswahilini linamgusa kwa namna moja ama nyingine … si linguine
ni swala hili la miziki ya kukesha ambayo
imejichukulia umaarufu kwa jina la vigodoro, kwa mtu anaye kaa mitaaa ya
mbezi beach, upanga au masaki ni vigumu kuelewa nachomaanisha lakini kwa watu
wa yombo vituka, tandale kwa tumbo , ukonga mazizini na sehemu kama tandika
wananielewa vizuri…
Ni ukweli
usiopingika kuwa hii ni kelo ya watanzania wengi hapa jijini, mara nyingi
miziki hii uanza siku ya alhamisi au ijumaa na kwenda mpaka jumapili… kero hii
inatokana na mtindo wa upigaji wa mziki huu usiozingatia mda ambapo upigwa
mpaka asubuhi bila kujali usumbufu mkubwa wanoupata watu wa karibu na vigodoro
hivyo…sasa pata picha umerudi toka kazini sa tano usiku kutokana na foleni
iliyopo mjini na unaamua kujipumzisha kidogo ili uwahi kuamka ukatafute riziki…
kwa sauti ya mziki huu sidhani kama utapata usingizi … kitu ambacho kinaweza
kupelekea uamke umechoka na ushindwe kufanya kazi zako kwa ufasaha,,,, hapa
tunaweza kusema kwamba miziki hii inarudisha nyuma maendeleo ya watanzania nan
chi kwa ujumla. Kero nyingine ya miziki
hii ya usiku ni ukiukwaji wa maadili ya mtanzania kwani kubali ukatae watu
wanacheza bila kuhofia chochote na mara nyingi kama unavyojua nyumba zetu za
uswahilini wengi hatuna mageti ya kuwazuia watoto wetu… watoto wengi wa umri wa
chini ya miaka kumi na nane wamekuwa wakitoroka nyumbani na kukimbilia kwenye
vigodoro hivo na kuwafanya wajifunze tabia ambazo ni zaidi ya umri wao.
Nadhani imefika
wakati sasa serikali kuangalia upya sharia za upigaji mziki katika kumbi za
starehe na majumbani.. mara nyingi sharia inasema baa zifungwe sa sita labda
uwe na kibali naalum kutoka sehemu husika .. lakini hii imekua ni tofauti kwa
vigodoro kwani uenda mpaka asubuhi na kusababisha kero isiyokuwa ya kawaida kwa
wakazi wa maeneo ya uswahilini
No comments:
Post a Comment