MADEMU WENGI SIO DILI, JAMAA APEWA KICHAPO CHA PAKA SHUME BAADA YA MADEMU ZAKE KUMFUMA AKIVINJARI.. MKASA HUU NOMA
Mkiambiwa
michepuko sio dili nyie mnakomaa mnajiona vidume kuwa na warembo
wengi.. katika hali ambayo iliwashangaa watu wengi na kuwaacha midomo
wazi wakazi wa mji wa kigamboni ni pale jamaa mmoja sharobaro mzuri tu
alipochezea kichapo baada ya
kugonganisha magari,, hapa wanaume viwembe mnaelewa naposema
kugonganisha magari.. inasemekana jamaa huyo anasoma chuo kimoja hapa
town na amekuwa na tabia ya kuwadump watoto wa kike.. shehuda wa tukio
hilo wanasema jamaa huyo aliingia katika nyumba yake ambapo amepanga na
wakati anaigia aliongozana na msichana mwembamba hivi.. na baada ya
masaa kama mawili alikuja dada ambaye alipakizwa kwenye bodaboda na
ndipo alipogonga na kufunguliwa mlango.. baada ya hapo watu walisikia
malumbano huko ndani mara
pakawa kimya na ndipo jamaa alapotoka akiwakimbiza mabinti hao huku
akivuja damu mdomoni na puani jambo lililohashiria kuwa jamaa alipewa
kichapo toka kwa wadada hao,,, hii nadhani ni fundisho kwa wengi wetu,
achana na michepuko la sivyo kama sio kukwaa ngoma huko maangaikoni
yatakukuta ya huyu jamaa
No comments:
Post a Comment